• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Wafanyakazi wa Kenya Airways watishia kufanya mgomo

    (GMT+08:00) 2018-10-23 20:12:51

    Wafanyakazi wa Shirika la ndege la Kenya, Kenya Airways wametishia kufanya mgomo mbele ya kuanzishwa kwa safari za moja kwa moja kati ya Nairobi na New York.

    Chama cha wahudumu wa usafiri wa anga (KAWU) kimesema wahudumu wake watagoma kwani shirika hilo limeshindwa kuamua malipo maalum kwa wahudumu kwenye safari ndefu ya kati ya Kenya na Marekani.

    Kawu kimesema mgomo huo utahusisha wahudumu hasa wa ndege aina ya Boeing 787 Dreamliner itakayotumika kwenye safari hizo.

    Hata hivyo mkurungezi mkuu wa shirika hilo Sebastian Mikosz amewaomba wahudumu hao kutogoa akisema baada ya kuzinduliwa kwa safari hizo watajadili kuhusu malipo maalum.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako