• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wateja wa tigo kuanza kulipia bidhaa na huduma mtandaoni

    (GMT+08:00) 2018-10-23 20:13:05

    Kampuni ya huduma za simu nchini Tanzaia ya Tigo imewawezesha wateja wake kuanza kutumia huduma za Tigo Pesa kulipia huduma na bidhaa mtandaoni.

    Mkuu wa huduma wa Tigo Pesa, Hussein Sayed amesema tangu Juni, Tigo ilikuwa inashirikiana na wataalamu wa kampuni ya Google ili kufanikisha malipo kwa kutumia huduma zao.

    Sayed amefafanua kuwa zaidi ya wateja milioni saba wa Tigo Pesa watakuwa na uwezo wa kupakua na kufurahia maudhui ya kimtandao kutoka Google Play Store ambayo yalikuwa yanalipiwa kwa kutumia kadi ya benki pekee.

    Mkurugenzi wa Google Afrika, Mahir Sahin amesema huduma hiyo itawawezesha mamilioni ya Watanzania ambao hawana kadi za benki kufurahia huduma za maudhui yanayopatikana kwenye Google Play.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako