• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Rwanda yasimamisha utafutaji wa mafuta kwenye ziwa la Kivu

    (GMT+08:00) 2018-10-23 20:13:50

    Serikali ya Rwanda imesimamisha mpango wake wa utafutaji wa mafuta kwenye ziwa la Kivu ili kupunguza hatari ya kupoteza fedha lakini imesema itaalika kampuni za kimataifa kufanya utafiti baadaye.

    Serikali imesema watafiti watarejea baada ya kukamilika kwa utafiti wa kijiolojia ili kubaini iwapo kuna manufaa ya kiuchumi ya kuingia kwenye ushirikiano na kampuni za kimataifa za mafuta.

    Mkurungezi wa halmashauri ya uchimbaji nchini Rwanda Francis Gatare amesema kwa sasa utafiti unaofanyika sio wa kina na unahusisha tu kuchimba visima vya mita kumi hivi na kufanyia upimaji kwenye maabara ili kuchunguza uwepo wa mafuta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako