• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Zaidi ya vijana 9,000 wanufaika na mradi wa ajira

    (GMT+08:00) 2018-10-23 20:14:06

    Zaidi ya vijana 9,000 wa kati ya miaka 16 na 30 wanaofanya kazi kwenye sekta ya jua-kali nchini Rwanda wameanza kunufaika na mradi wa ajira uanaofadhiliwa na Umoja wa Ulaya.

    Wanaofaidika ni vijana kama vile wachuuzi, waendesha bodaboda za baiskeli, wasusi na wafanyakazi kwenye machimbo.

    Waliolengwa kwenye sekta ya madini wako kwenye wilaya za Nyarugenge, Kicukiro, Rubavu, Nyabihu, Ngororero, Gekenke na Rulindo.

    Ufadhili huo wa dola milioni 2.1 ulitolewa baada ya utafiti kubaini kwamba asilimia 50 ya wale wanaofanya kazi kwenye sekta ya jua kali wanapata chini ya nusu dola kwa siku.

    Chini ya mpango huo vijana waliwezeshwa kupata mafunzo na baada ya kuhitimu kupewa vifaa vya kufanyia kazi yenye mapato ya juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako