• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kuogelea: Rwanda yaja mikakati mipya ili kuibua vipaji vipya

  (GMT+08:00) 2018-10-24 08:37:39

  Shirikisho la mchezo wa kuogelea nchini Rwanda RSF limeweka wazi mipango yake kwa ajili ya maendeleo ya mchezo huo, ambapo limetangaza kuanzisha mashindano mapya ya kikanda na kitaifa.

  Mashindano mapya yatalenga zaidi kuzalisha vipaji vipya vya mchezo huo, likiwemo zoezi la kuanzisha mashindano ngazi ya shule, yatakayoshirikisha vijana chini ya umri wa miaka 17 wanaume na wanawake, na mashindano maalum ya kitaifa ya kuogelea kwa vijana chini ya umri wa miaka 21 ambayo yatakuwa yakifanyika kila ifikapo mwezi Disemba.

  Katika hatua nyingine RSF limetoa kalenda ya mwaka 2019 yenye ratiba za mashindano ya kuogelea, na michezo mbalimbali ya kwenye maji inayosimamiwa na shirikisho hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako