• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makamu wa rais wa China akutana na waziri mkuu wa Palestina

    (GMT+08:00) 2018-10-24 10:12:51

    Makamu wa rais wa China Bw. Wang Qishan ambaye yupo ziarani nchini Palestina jana huko Ramallah alikutana na waziri mkuu wa Palestina Bw. Rami Hamdallah.

    Bw. Wang alisema China inaunga mkono Palestina kutatua mgogoro na Israel kwa njia ya mazungumzo, na itaendelea kuhimiza suala la Palestina kutatuliwa kwa haki kutokana na "mpango wa nchi mbili". Aliongeza kuwa China inafurahia Palestina kujiunga na pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na itahimiza kampuni za China kuwekeza nchini Palestina.

    Naye Bw. Hamdallah alisema Palestina inaishukuru China kwa kuwa na msimamo wenye haki katika suala la Palestina, na kutumai China kutoa mchango zaidi katika mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako