• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Daraja la Hongkong-Zhuhai-Macao kuhimiza maendeleo ya Hongkong, Macao na sehemu Magharibi ya Delta ya Zhujiang

  (GMT+08:00) 2018-10-24 16:43:42

  Daraja la Hongkong-Zhuhai-Macao limezinduliwa rasmi jana, daraja hilo si kama tu litahimiza uchumi na biashara na mawasiliano ya watu wa sehemu hizo tatu, bali pia litahimiza maendeleo ya Hongkong, Macao na sehemu Magharibi ya Delta ya Zhujiang.

  Mkuu wa Mkoa wa utawala maalumu wa Hongkong Bi. Lam Cheng Yuet-ngor jana kwenye sherehe ya uzinduzi wa daraja la Hongkong-Zhuhai-Macao amesema, ujenzi wa miundombinu ya kuvuka mipaka umetoa msingi mzuri kwa ujenzi wa eneo kubwa la Guangdong, Hongkong na Macao, na kuzinduliwa kwa daraja hilo kutatia nguvu mpya ya kuhimiza maendeleo ya Hongkong kwa pande nyingi.

  Hongkong imeonesha umuhimu wa kuwa mlango kwa biashara za uagizaji na usafirishaji za China. Kutokana takwimu zilizotolewa na serikali ya Hongkong, asilimia 15 ya thamani ya jumla ya uagizaji wa China kutoka nje mwaka 2017 ilikamilishwa kwa kupitia Hongkong.

  Bw. Zhang Xuexiu ni mkuu wa Idara ya Biashara ya nje na usafirishaji mkoani Hongkong, anafahamu umuhimu wa mawasiliano ya barabara kwa maendeleo ya viwanda na biashara. Bw. Zhang amesema, daraja la Hongkong-Zhuhai-Macao ni daraja linaloweza kuleta fursa za biashara. Anasema,

  "Baada ya kuzinduliwa kwa daraja hilo, mawasiliano kati ya Hongkong, Macao na Guangdong ni rahisi zaidi, na fursa za uwekezaji pia zitaongezeka zaidi, tunaweza kubadilishana habari nyingi zaidi za uwekezaji. Daraja hili linaweza kupunguza muda wa usafiri kati ya sehemu hizo tatu, watu wengi watachagua kwenda China bara, na marafiki wengi zaidi wa Guandong watachagua kuja Hongkong na Macao."

  Bw. Zhang anasema, miaka 90 ya karne iliyopita aliwahi kuanzisha kiwanda huko Zhuhai, lakini baadaye alifunga kiwanda hicho kutokana na usafirishaji wa bidhaa kuwa mgumu na gharama kubwa, na kuhusu kama atazingatia upya kuwekeza Zhuhai au la, Bw. Zhang anasema:

  " Bila shaka nitazingatia. Zamani tuliona Zhuhai ni mahali mazuri pa kutalii na kuishi, lakini hapafai kwa kufanya biashara kutokana na miundombinu mibaya ya mawasiliano. Lakini hivi sasa baada ya kuzinduliwa kwa daraja hilo, si kama tu tutakwenda pale kuishi, kutalii, bali pia tutakwenda kuwekeza. Kwa pande hizo, Zhuhai ni mahali panapofaa. "

  Daraja la Hong Kong- Zhuhai-Macao lenye urefu wa kilomita 55 ni daraja refu zaidi la kuvuka bahari duniani. Mbunge wa Hongkong kutoka sekta ya utalii Bw. Yao Sirong anasema, daraja hilo lenyewe ni mvuto wa utalii. Anasema, kabla ya kuzinduliwa kwa daraja hilo, sekta ya utalii ya China Bara ilianza kuandaa taratibu za utalii kwenye daraja hilo, na sekta ya utalii ya Hongkong pia iliandaa shughuli kadhaa, na watu wote wanapenda kutembelea daraja hilo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako