• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Maonesho ya kwanza ya mawasiliano ya sanaa ya "Ukanda Mmoja na Njia Moja" kati ya Afrika na China yafunguliwa nchini China

    (GMT+08:00) 2018-10-24 16:51:05

    Maonesho ya kwanza ya mawasiliano ya sanaa ya "Ukanda Mmoja na Njia Moja" kati ya Afrika na China yaliyoandaliwa na wizara ya michezo, sanaa na utamaduni ya Kenya yamefunguliwa kwenye maktaba ya taifa ya China.

    Akihutubia kwenye ufunguzi huo, Mkurugenzi wa wizara hiyo Dkt Kiprop Lagat amesema, pendekezo la "Ukanda Mmoja na Njia Moja" lililotolewa na China limeinufaisha Kenya, akitolea mfano wa reli ya SGR, na kwamba maonesho hayo ni mafanikio yaliyopatikana chini ya pendekezo hilo. Pia ameyataka maonesho hayo yaweze kuwavutia marafiki wengi zaidi kwenda nchini Kenya kuangalia na kuhisi ukarimu wa watu wa Afrika.

    Maonesho hayo yenye kaulimbiu ya "Kuingia Kenya, Kufahamu Afrika Mpya" yanaonesha michoro na sanamu zaidi ya 110 kutoka kwa wasanii zaidi ya 40 wa nchi mbalimbali za Afrika ikiwemo, Kenya, Rwanda, Uganda, Zimbabwe na Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako