• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la maonesho ya kimataifa ya Njia ya Hariri Baharini ya mwaka 2018 kufanyika Guangzhou

    (GMT+08:00) 2018-10-24 16:58:19

    Baraza la maonesho ya kimataifa ya Njia ya Hariri Baharini ya karne ya 21 ya mwaka 2018 litafanyika ijumaa huko Guangzhou.

    Viongozi wa zamani na mawaziri wa nchi 15 kutoka nchi za Ukanda Mmoja na Njia Moja, wadau wa mashirika ya biashara ya nchi 28 na wadao wa mashirika ya husika ya kimataifa, wataalamu hodari wa uchumi wa kimataifa, viongozi wa sekta ya biashara wa China na nchi za nje wanatarajiwa kuhudhuria baraza hilo.

    Kauli mbiu ya Baraza hilo ni uvumbuzi na kufungua jukwaa jipya la ushirikiano na kuongeza nguvu mpya ya maendeleo ya pamoja. Licha ya baraza kuu, mikutano mingine itafanyika ikiwemo baraza la ujenzi wa eneo la Dawan la Guangdong-Hong Kong-Macao na Ukanda Mmoja na Njia Moja, baraza la ushirikiano na maendeleo ya ujenzi wa eneo la viwanda la Ukanda Mmoja na Njia moja, na baraza la mafunzo ya watu wanaofanya kazi za kufundisha kichina kwenye nchi za Ukanda Mmoja na Njia Moja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako