• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Matumizi ya gesi asilia Tanzania yaokoa $10.29bn

    (GMT+08:00) 2018-10-24 20:46:15

    Matumizi ya gesi asilia katika kuzalisha umeme nchini Tanzania yameokoa kiasi cha $10.29bn (Tsh23.56 trilioni) ambazo zingetumika kununua mafuta nje ya nchi kwa ajili ya kuzalisha umeme tangu mwaka 2004 hadi Septemba 2018.

    Hayo yalielezwa jana jijini Dodoma na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) ,Mhandisi Kapuulya Musomba ,wakati akiwasilisha taarifa kuhusu mchango wa gesi asilia katika uzalishaji wa umeme kwa wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

    Mhandisi Musomba alisema kwa kipindi cha kuanzia mwaka 2004 hadi Septemba 2018 ,gesi asilia kiasi cha futi za ujazo bilioni 381 kilitumika kuzalisha umeme pekee ambapo hadi kufikia Septemba 2018,mitambo yenye uwezo wa kuzalisha umeme wa jumla ya megawati 831 kwa siku kutokana na gesi asilia imewekezwa nchini Tanzania.

    Aliongeza kuwa zaidi ya silimia 50 ya umeme unaozalishwa nchini humo unatokana na gesi asilia huku vyanzo vingine vya uzalishaji umeme vikiwa ni maji,nishati jadidifu na mafuta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako