• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya Samsung yafungua makao makuu katika jumba la Two Rivers,Kenya

    (GMT+08:00) 2018-10-24 20:46:53

    Kampuni ya simu ya Samsung imefungua duka kubwa zaidi barani Afrika katika jumba la maduka la Two Rivers jijini Nairobi,nchini Kenya.

    Kulingana na rais wa Samsung Sung Yoon, hatua hiyo ilikuwa ni katika sehemu ya mikakati yake ya kulainisha operesheni zake za kibiashara Afrika kwa lengo la kuimarisha ufanisi wake katika mauzo na huduma zake kwa wateja.

    Aidha alisema kufunguliwa kwa duka hilo kutawapa wateja huduma wanayohitaji.

    Duka hilo litauza bidhaa za kielektroniki na simu na pia kitakuwa ni kituo cha kutoa huduma kwa wateja.

    Kufikia sasa, Samsung ina maduka 29 nchini Kenya katika miji ya Nairobi, Kisumu, Mombasa, Meru, Nakuru, Thika na Kitengela.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako