• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FIFA kuipa Kenya Sh100 milioni kuinua soka ya wanawake

    (GMT+08:00) 2018-10-25 09:11:28

    Shirikisho la Soka la Kenya (FKF) limesema kuwa shirikisho la soka duniani (FIFA) linapanga kuipa shilingi milioni 101,210,000 za Kenya kuimarisha soka ya wanawake baada ya kuridhishwa na mipango yake.

    Rais wa FKF Nick Mwendwa amesema jijini Nairobi kwamba FIFA imeamua kuitengea Kenya fedha hizo baada ya kuiona inachukulia soka ya wanawake kwa uzito.

    Aidha, Mwendwa amesema kwamba Kenya itawekeza sehemu ya fedha hizo katika kufundisha makocha wa timu za wanawake. Idadi kubwa ya klabu za wanawake nchini Kenya zinapata mafunzo kutoka kwa makocha wanaume. Hata timu ya taifa ya wanawake ya Kenya Harambee Starlets, ambayo imefuzu kushiriki Kombe la Afrika (AWCON) nchini Ghana mwezi ujao, iko chini ya kocha mwanamume David Ouma.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako