• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Aliyempiga McGregor yupo tayari kuzipiga na 'Money' Mayweather, pambano kufanyika Moscow

    (GMT+08:00) 2018-10-25 09:12:38

    Bingwa wa UFC, Khabib Nurmagomedov amesema kuwa yupo tayari kupigana na mwanamasumbwi Floyd Mayweather huku akihitaji pambano hilo lifanyike jijini Moscow Urusi.

    Nurmagomedov raia wa Urusi ni mpiganaji anayetumia 'martial artist' anahitaji kupigana na Mayweather ambaye tayari alishampiga Conor McGregor katika pambano lililoingiza pesa nyingi.

    Mayweather ambaye alishatangaza kustaafu alirejea tena ulingoni na kumpiga McGregor mwaka 2017 na kuweka rekodi yake sawa ya kushinda jumla ya mapambano 50-0 bila kupigwa hata moja.

    Kama pambano hilo litafanyika jijini Moscow kama Nurmagomedov alivyosema basi itakuwa ni mara ya kwanza kwa Mayweather kupigana nje ya Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako