• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Roman Reigns augawa mkanda wa WWE

  (GMT+08:00) 2018-10-25 09:26:35

  Baada ya nyota wa mieleka duniani Roman Reigns kutangaza kuwa anaumwa Saratani, shirikisho la mchezo huo duniani WWE limempa pole na kuweka wazi kuwa hatashiriki tena fainali ya kuwania mkanda wa dunia.

  WWE wamethibitisha kuwa mwanamieleka huyo anaumwa saratani ya damu yaani 'Leukemia' inayoshambulia chembechembe nyeupe za damu.

  Roman mwenye miaka 33 kwa sasa ndiye anayeshikilia mkanda wa dunia wa mchezo huo, alizungumza katika jukwaa na kusema kuwa hatashindana kugombea mkanda huo ila atarejea baadaye iwapo afya yake itaimarika.

  Kwa mujibu wa bosi wa WWE, Vince McMahon mkanda wa dunia sasa utawaniwa na wanamieleka wawili tu badala ya watatu ambao ni Brock Lesnar na Braun Strowman, Novemba 2, mwaka huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako