• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kongamano la 8 la Xiangshan lafunguliwa mjini Beijing

    (GMT+08:00) 2018-10-25 15:37:46

    Kongamano la 8 la Xiangshan limefungua leo katika kituo cha mikutano ya kimataifa cha Beijing, ambapo Waziri wa ulinzi wa China Bw. Wei Fenghe amesoma barua ya pongezi kwa kongamano hilo kutoka rais Xi Jinping wa China.

    Katika barua hiyo, rais Xi ameeleza msimamo wa China wa kuongeza uaminifu wa kimkakati na nchi mbalimbali na nia ya dhati ya kuimarisha ushirikiano wa kulinda usalama. Pia rais Xi ameweka wazi uamuzi wa China katika kujiendeleza kwa njia ya amani na kujitahidi kujenga jumuiya ya binadamu yenye hatma ya pamoja.

    Bw. Wei amesema, jeshi la China litaendelea kufuatilia msimamo wa kulinda uhuru, usalama na maendeleo ya taifa na amani ya dunia, na kwamba jeshi hilo linapenda kushirikiana na majeshi ya nchi mbalimbali kusukuma mbele ujenzi wa mfumo mpya wa usalama wa kanda ya Asia na Pasifiki, kuimarisha ushirikiano wa kijeshi na nchi jirani na nchi zinazoendelea, kuongeza mazungumzo ya usalama na majeshi ya nchi mbalimbali, na kujenga uhusiano mpya kati ya nchi mbalimbali ili kutoa mchango mkubwa zaidi katika kulinda kwa pamoja amani na utulivu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako