• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda kuwezesha vijana elfu 9 kwa mikopo

    (GMT+08:00) 2018-10-25 20:02:39

    Zaidi ya vijana elfu 9 kati ya umri wa miaka 16 na 30 wanaofanya kazi katika sekta ya juakali nchini Rwanda,sasa watapata mikopo kutoka kwa umoja wa ulaya.

    Watakaofaidika ni pamoja na wachuuzi,madereva wa taxi,wafanyikazi wa nyumbani,wahudumu wa mikahawa,wakulima na wahudumu wa vinyozi na saloon.

    Msaada huu wa Euro milioni 2.1 unalenga kuimarisha maisha ya watu wa rwanda ambao hawajaajiriwa rasmi.

    Mkurugenzi wa mradi huo Rwanda Stefano Manservisi amewataka wahusika kujisajili na vyama vya ushirika .

    Fauka ya fedha ,watapewa mafunzo ya taaluma zao na maelezo muhimu ya kujiinua kifedha .

    Mradi huo wa miaka 5 utaanza Disemba na kufikishwa katika maeneo ya mashambani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako