• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Punguzeni mawaziri na wabunge tupate ajira ,wanauchumi wadai

    (GMT+08:00) 2018-10-25 20:03:19

    Serikali ya Uganda imetakiwa kupunguza idadi ya mawaziri,wabunge,wakuu wa wilaya na viongozi wengine ili kufungua fursa za ajira na kuokoa fedha.

    Profesa John Ddumba mwanauchumi na mhadhiri wa Chuo kikuu cha Makerere amekosoa utendakazi wa viongozi akisisitiza kwamba fedha hizo zinapaswa kutumika kwenye miradi ya ajira na maendeleo ya vijana .

    Hivi karibuni tetesi nyingi zimezuka za vijana kuteseka na kufariki wakifanya kazi katika nchi za mashariki ya kati.

    Wanauchumi wameshinikiza kwamba ukosefu wa ajira umechangia ongezeko la vijana kusafiri nchi hizo za mateso kutafuta ajira.

    Msemaji wa serikali ya Uganda Ofwoni Opondo hata hivyo amesema idadi ya wawakilishi wa serikali sio sababu za ukosefu wa ajira na kupendekeza sekta binafsi inapaswa kuongeza fursa za ajira kwa vijana.

    Vijana wengi wanaohitimu kutoka vyuo vikuu wamekosa kazi kutokana na ukosefu wa fedha na miradi ya maendeleo.

    Vijana sasa wameanzisha kampeini za kulazimisha ajira .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako