• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujumbe wa CAF wazuru Qatar, kutathimini maandalizi ya Kombe la dunia

    (GMT+08:00) 2018-10-26 13:02:29

    Ujumbe wa Shirikisho la kandanda barani Afrika (CAF) umezuru nchini Qatar kujionea maandalizi ya nchi hiyo kuelekea fainali za Kombe la dunia za mwaka 2022.

    Ujumbe huo umeongozwa na rais Ahmad Ahmad na umekutana na rais wa Shirikisho la kandanda nchini Qatar (QFA) Sheikh Hamad bin Khalifa bin Ahmed Al Thani.

    Mbali na kujadili kuhusu fainali za Kombe la dunia pia viongozi hao wamejadili kuhusu miradi mbalimbali soka inayotekelezwa na pande hizo mbili.

    Mkutano huo ni utekelezaji wa makubaliano baina ya taasisi hizo mbili kuhusu maendeleo ya mchezo wa soka yaliyotiliwa saini mwaka 2015 wakati huo CAF ikiongozwa na Issa Hayatou.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako