• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tenisi: Mserbia amtoa jasho kigogo Federer

    (GMT+08:00) 2018-10-26 13:03:19

    Mchezaji tenisi namba tatu kwa ubora duniani, Roger Federer wa Uswisi, juzi aliponea chupuchupu kuadhiriwa na mchezaji chipukizi, Filip Krajinovic wa Serbia.

    Federer alilazimika kufanya kazi ya ziada kupata ushindi wa seti mbili kwa moja 6-2, 4-6, 6-4 katika raundi ya pili ya mashindano ya Swiss Indoorsn yanayofanyika kwenye Uwanja wa St. Jakobshalle.

    Mchezaji huyo alikaribia kukumbwa na aibu iliyompata katika mashindano kama hayo mwaka 1998, alipotolewa raundi ya kwanza na kinda anayeshika nafasi zaidi ya 200 kwa viwango vya ubora duniani.

    Amesema mchezo huo umempa funzo na atakuwa makini katika mechi zijazo anapocheza na mchezaji asiyekuwa na jina au mwenye kiwango bora.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako