• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pato la kampuni zinazoendeshwa na serikali kuu ya China laongeza kwa asilimia 19.1 katika robo tatu ya mwanzo ya mwaka huu

    (GMT+08:00) 2018-10-26 18:56:23

    Takwimu zilizotolewa na Wizara ya Fedha ya China zimeonesha kuwa, pato la kampuni zinazoendeshwa na serikali kuu ya China limeendelea kuongezeka katika miezi tisa ya mwaka huu, lakini kasi ya ongezeko hilo imepungua kidogo.

    Pato la kampuni hizo limefikia dola za Marekani bilioni 371 katika robo tatu ya mwanzo ya mwaka huu, ambalo limeongeza kwa asilimia 19.1 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu. Lakini ongezeko hilo limepungua ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 20.7 la kampuni hizo katika miezi minane ya mwanzo ya mwaka huu.

    Habari zinasema, mpaka mwishoni mwa mwezi wa Septemba, thamani ya kampuni hizo zimefikia dola za Marekani trilioni 25.2 ambayo imeongeza kwa asilimia 8.6 kuliko ya mwaka jana, ambapo madeni yao yamefikia dola za Marekani trilioni 16.4.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako