• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mashirika ya kilimo yaitaka Kenya kuongeza ufadhili wa kilimo

    (GMT+08:00) 2018-10-26 19:15:20

    Wasimamizi wa mashirika ya kilimo nchini Kenya wameitaka serikali kuongeza ufadhili wa kilimo hadi asilimia 15 ya mapato ya kitaifa. Aidha, wamezitaka serikali za kaunti kuhakikisha kuwa bajeti zao zinafadhili shughuli za kilimo kwa asilimia 10 ili kuafjikia lengo kuu la uhuru la kupambana na njaa.

    Kitaifa, asilimia hiyo itagonga 25 kinyume na hali ya sasa ambapo kilimo hupewa kati ya asilimia tatu na saba ya mapato ya kitaifa.

    Mwenyekiti wa muungano wa wakulima wa nafaka nchini Kenya (KCGA) Bw James Irungu alisema kuwa kiini cha kuweko kwa makali ya njaa miaka 55 baada ya uhuru ni kutokuweko na sera mwafaka za kuimarisha uzalishaji wa chakula cha kutosha kwa lishe ya jamii.

    Alisema kuwa sera za Wizara ya Kilimo hapa nchini zimekuwa zikizingatia kwa kiwango kikuu jinsi ya kukuza mazao ya kuuza sokoni huku ikikosa kutiliwa maanani chakula kwa jamii. Alisema kuwa kile kitakachookoa taifa hili ni ufadhili wa kutosha katika safu za unyunyiziaji, vifaa vya kilimo na mimea iliyofanyiwa utafiti wa kunawili katika hali ngumu za mazingara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako