• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkataba wa mgawanyo wa uzalishaji mafuta ya gesi wasainiwa Zanzibar

    (GMT+08:00) 2018-10-26 19:15:41

    Ushirikiano wa Rais wa Zanzibar, Dkt Ali Mohamed Shein na Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ndio umewezesha utiaji saini mkataba wa mgawanyo wa uzalishaji wa mafuta na gesi asilia visiwani humo. Dkt Shein alisema hayo wakati wa utiaji saini mkataba huo uliofanyika kati ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) na kampuni ya Rakgas ya Ras Al Khaimah.

    Mkataba huo unahusisha kitalu maalumu kinachohusisha eneo la nchi kavu ya Zanzibar na sehemu ya eneo la bahari. Mikataba mingine kama hiyo itakayofuata itahusisha maeneo ambayo yamo katika hatua za matayarisho.

    Dkt Shein alitoa siri hiyo kutokana na suala la mafuta kuwamo ndani ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano, ambapo awali lilisababisha mivutano ya kisheria miongoni mwa wanasiasa. Alisema kutokana na hilo, alishirikiana na Rais Kikwete kufikia na kuandaa njia bora itakayowezesha pande mbili za Muungano kusimamia rasilimali za mafuta na gesi asilia kwa utaratibu wa kisheria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako