• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali kurejesha treni jijini kupunguza msongamano

    (GMT+08:00) 2018-10-26 19:16:29

    Serikali ya Kenya imetangaza kuanzisha mpango wa kuanzisha tena uchukuzi kwa njia ya treni Jijini Nairobi.

    Waziri wa Uchukuzi James Macharia Jumanne alisema serikali imechagua kuanzisha magari mengi ya moshi badala ya mabasi kwa lengo la kupunguza msongamano jijini.

    Bw Macharia alisema makatibu wakuu kutoka Wizara ya Uchukuzi na Muundo Msingi tayari wameenda Uhispania kwa lengo la kumalizia ununuzi wa magari hayo.

    Ameongeza kuwa kwa sasa wanalenga njia mbili, moja ni ile ya Syokimau hadi katikati mwa jiji na nyingine ni ile ya Ruiru hadi katikati mwa jiji. Macharia alisema njia hizo mbili zitatoa uchukuzi mbadala baada ya kusimamisha mpango wa kuanzisha uchukuzi kwa njia ya mfumo maalum wa Rapid Transit System –RTS.

    Hata hivyo, alisema magari hayo sio eti yanachukua mahali pa mabasi hayo (Bus Rapid Transit-BRT).

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako