• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri Mkuu Li atoa wito wa kuimarishwa mawasiliano na ushirikiano katika kuendeleza elimu ya viumbe hai

    (GMT+08:00) 2018-10-27 19:10:41

    Waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang leo jumamosi ameeleza umuhimu wa kuimarisha mawasiliano, kujenga maelewano na kuinua ushirikiano ili kupata mafanikio zaidi kwenye utafiti na uvumbuzi wa kiteknolojia kuhusu elimu ya viumbe hai.

    Bw. Li Keqiang ametoa maoni hayo kwa njia ya maelezo yaliyoandikwa kwenye hafla ya ufunguzi wa mkutano kuhusu elimu ya viumbe hai duniani WLSC unaofanyika hapa Beijing.

    Aidha, Waziri Mkuu Li amesema, kwa kuwa nchi nyingi zinaangazia elimu ya viumbe, mada kuhusu afya na maendeleo ya binadamu, kama eneo muhimu kwenye sayansi na uvumbuzi wa kiteknolojia, sasa inakabiliwa na fursa kubwa za kimaendeleo kuliko hapo awali.

    China pia imeimarisha maendeleo ya elimu ya viumbe hai, na inatilia umuhimu zaidi kuvumbua teknolojia mpya na sekta zinazohusiana na mada hiyo.

    Aidha Waziri Mkuu Li ametoa wito kwa wataalam wanaohudhuria kuungana kwa pamoja katika kuzikabili changamoto kama vile magonjwa hatari, ongezeko la idadi ya wazee, uchafuzi wa mazingira na upungufu wa uwezo, ili kuimarisha maendeleo endelevu katika uchumi wa dunia na jamii, na maendeleo ya binadamu duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako