• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kazi za Sanaa kutoka Afrika zaonyeshwa mjini Beijing

  (GMT+08:00) 2018-10-28 18:26:51

  Onyesho la kazi mbalimbali za Sanaa zilizofanywa na wasanii wa Afrika na China lilifunguliwa wiki hii katika maktaba ya taifa ya China.

  Onyesho hilo ambalo ni sehemu ya mpango wa kwanza wa utekelezaji wa pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja kuhusu mabadilishano ya Sanaa kati ya Afrika na China, na baraza la utamaduni kati ya China na Afrika, liliandaliwa kwa pamoja na Wizara ya michezo, utamaduni na Sanaa ya Kenya, Chama cha ushirikiano wa utamaduni wa Afrika na China, pamoja na maktaba ya taifa ya China.

  Zaidi ya nusu ya kazi 110 za sanaa zilizoonyeshwa, zikiwemo michoro ya rangi, michoro ya chaki na vinyago, ziliandaliwa na zaidi ya wasanii 40 kutoka Afrika, wakiwemo kutoka Kenya, Rwanda, Zimbabwe na Tanzania.

  Wasanii kutoka China zaidi waliandaa kazi ambazo zinaonyesha utekelezaji wa pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja na maisha ya sasa ya kiafrika.

  Mkurugenzi wa Idara ya Utamaduni kutoka wizara ya Michezo, Utamaduni na Sanaa ya Kenya Bw. Kiprot Lagat amesema Kenya imenufaika sana kutokana na maendeleo ya pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja, na alieleza matumaini kutokana na maonyesho hayo, kwa kuwa watu wengi zaidi kutoka China watavutiwa kwenda Kenya ili kujua ukarimu wa watu Kenya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako