• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ligi Kuu Tanzania Bara-Simba yamjibu Masau kwa vitendo, yapiga mkono, Okwi afunga Hat Trick

  (GMT+08:00) 2018-10-29 10:39:37

  Timu ya Simba ya Dar es salaam umemjibu msemaji wa timu ya Ruvu Shooting Masau Bwire kwa vitendo baada ya kuifunga Ruvu Shooting kwa magoli 5-0 maarufu kama mkono. Katika mchezo wa ligi kuu Tanzania bara uliopigwa jana jijini Dar.

  Kabla ya mechi hiyo Bwire alisema timu yake imepata mbinu ambayo ingeushangaza ulimwengu kwa kuweza kuwafunga mabingwa hao watetezi na kuwafanya waulize wanakokaa hali ambayo iliwafanya viongozi wa Simba kutulia.

  Mshambuliaji toka Uganda anayechezea klabu hiyo ya simba Emmanuel Okwi alifunga mabao 3, huku mnyarwanda Meddie Kagere akipachika bao moja na Adam Salamba akishindilia msumari kwa kupachika bao la tano.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako