• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Shujaa katika kundi moja na Fiji, Ufaransa na Scotland –Dubai Sevens

    (GMT+08:00) 2018-10-29 10:40:18

    Timu ya taifa ya raga wachezaji saba kila upande ya Kenya (Shujaa) italimana na Fiji, Ufaransa na Scotland katika mechi za kundi B za duru ya ufunguzi ya michuano ya raga ya dunia ya msimu 2018-2019 ya Dubai Sevens itakayoanza Novemba 30 na Desemba 1, 2018. Droo ilitangazwa na Shirikisho la Raga Duniani (World Rugby) Oktoba 25.

    Michuano ya raga ya dunia ya msimu huu inatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa. Timu 15 zinazoshiriki duru zote 10 za ligi zitawania kutwaa ubingwa. Mataifa manne ya kwanza pia yatafuzu kushiriki michezo ya Olimpiki mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako