• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Ufaransa wapongezana kwa kurusha kwa pamoja satelaiti iliyosanifiwa na nchi hizo

    (GMT+08:00) 2018-10-29 19:52:01

    Rais Xi Jinping wa China na rais Emmanuel Macron wa Ufaransa wametumiana salamu za pongezi kwa kurushwa kwa mafanikio satelaiti ya kufuatilia mwenendo wa bahari iliyosanifiwa kwa pamoja na nchi hizo mbili.

    Jukumu hilo la pamoja kati ya Idara ya taifa ya Anga za Juu ya China na na Kituo Kikuu cha Safari za Anga ya juu cha Ufaransa, litawezesha usimamizi wa saa 24 wa mwenendo wa mawimbi, ukubwa wake na mawimbi ya juu ya bahari.

    Rais Xi amesema, ushirikiano wa anga ya juu ni sehemu muhimu ya uhusiano wa kimkakati wa China na Ufaransa, na kurushwa kwa mafanikio kwa satelaiti hiyo kunawakilisha matokeo ya hivi karibuni ambayo yatachukua nafasi muhimu katika usimamizi wa bahari duniani.

    Kwa upande wake, rais Macron amesema kurushwa kwa satelaiti hiyo ni hatua muhimu ya ushirikiano wa pande mbili katika masuala ya anga za juu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako