• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Zipline kufungua kiwanda Rwanda

    (GMT+08:00) 2018-10-29 20:33:24
    Kampuni ya Zipline ya Marekani ambayo inatengeneza ndege ambazo hazina rubani yaani Drones, imesema inapanga kufungua kiwanda cha kuuunganisha ndege hizo nchini Rwanda.

    Zipline ncfio kampuni ya pekee duniani inayotengeneza ndege za kuwasilisha bidhaa na nchini Rwanda zimeanza kutumika kutuma damu na dawa katika setka ya afya.

    Zipline ilizindua oparesheni zake katika wilaya ya Muhanga kusini mwa Rwanda miaka mwili iliopita na imekuwa ikilipwa na wizara ya afya baada ya kuwasilisha bidhaa.

    Wiki iliopita baraza la mawaziri nchini humo liliidhinisha makubaliano ya kuongeza kandarasi yao kwa miaka mingine mitatu.

    Waziri wa afya nchini humo Dkt. Diane Gashumba, amesema huduma za Zipline zimekuwa zikitumika kuwasilisha dawa na damu inayohitajika kwa dharura kwa hospitali 19.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako