• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yapaa nafasi ya nane kwa nchi zilizovutia wawekezaji.

    (GMT+08:00) 2018-10-29 20:34:35

    Tanzania imeshika nafasi ya nne kwa nchi zilizovutia wawekezaji

    Kutokana na uimarishaji wa miundombinu unaoendelea, Afrika Mashariki imetajwa kuongoza kwa kuvutia wawekezaji, ripoti ya Ernst & Young (EY) imebainisha.

    Ripoti hiyo inasema hali hiyo imechangiwa na ujenzi wa miradi mikubwa unaofanywa katika sekta za miundombinu, teknolojia, ukarimu na nyumba za makazi.

    Miradi mikubwa inayoendelea kutekelezwa Tanzania, Ethiopia, Kenya, Uganda na Rwanda, ripoti inasema imeifanya Afrika Mashariki kutupiwa macho zaidi na wawekezaji wengi duniani.

    Hali hiyo umeufanya Ukanda wa Afrika Mashiriki kuongoza kwa mara ya kwanza, kwa kuvutia miradi mingi zaidi ya uwekezaji wa moja kwa moja kutoka nje (Foreign Direct Investment - FDI) kuliko ukanda mwingine wowote barani Afrika.

    Kwa mara ya kwanza, ripoti hiyo ijulikanayo kama 'The Africa Attractiveness Report 2018' inasema: Mwaka jana, Afrika Mashariki ilikaribisha miradi 197 tofauti na 185 iliyokuwapo Kaskazini au 172 ya Magharibi na 162 ya Kusini mwa Afrika. Miradi 197 ya Afrika Mashariki ni sawa na ongezeko la asilimia 82 ikilinganishwa na iliyosajiliwa mwaka 2016. Kenya, Ethiopia na Tanzania zilisajili miradi mingi zaidi mwaka jana baada ya kupokea miradi kwa uwiano wa 67, 62 na 35.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako