• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Starlets kupimana ubavu na Ghana Novemba 7

    (GMT+08:00) 2018-10-30 08:54:50
    Timu ya taifa ya wanawake ya Kenya Harambee Starlet, imepata uhakika wa kucheza mechi mbili za kujipima ubavu ikiwa ni sehemu ya maandalizi kabla ya kuelekea Ghana kwa ajili ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika (AWCON) yatakayotimua vumbi kuanzia Novemba 17 hadi Desemba mosi.

    Timu ya taifa ya wanawake ya Ghana Black Queens imekubali mwaliko wa kucheza mechi ya kirafiki ikiwa ni siku chache baada ya timu ya taifa ya wanawake ya Uganda (Crested Cranes) kukubali ombi la kukipiga na Starlets.

    Ghana itasafiri hadi Nairobi na kuumana na Kenya Novemba 7 katika uwanja wa Kasarani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako