• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ujenzi wa Eneo la kitaifa la majaribio ya maendeleo ya kilimo la Weifang lahimiza ufunguaji mlango wa kilimo kwa nje

    (GMT+08:00) 2018-10-30 18:16:59

    Eneo la kitaifa la majaribio ya maendeleo ya kilimo la Weifang mkoani Shandong limeidhinishwa rasmi kujengwa. Mkuu anayeshughulikia kilimo na vijiji wa Idara ya ushirikiano wa kimataifa ya China Bw. Sui Pengfei ametangaza kuwa, China si kama tu itazidi kupanua ufunguaji mlango kwenye mambo ya kilimo na vijiji kupitia ujenzi wa eneo hilo, bali pia itaharakisha uvumbuzi wa mfumo nchini, pamoja na mchakato wa mageuzi ya kilimo.

    Mwezi Julai mwaka 2017, Wizara ya kilimo na vijiji ya China iliidhinisha maeneo 10 ya vielelezo ya ushirikiano wa kilimo nje ya China, pamoja na maeneo 10 ya majaribio ya ushirikiano na ufunguaji mlango wa mambo ya kilimo. Baada ya juhudi za mwaka mmoja, Baraza la serikali la China limeidhinisha ujenzi wa eneo shirikishi la majaribio la ufunguaji mlango na maendeleo la kitaifa la Weifang. Bw. Sui Pengfei anasema:

    Katika zama mpya, ufunguaji mlango katika mambo ya kilimo unapaswa kuzingatia uvumbuzi na ushirikiano na nje."

    Mwaka 2018 ukiwa ni mwaka wa tano tangu China itangaze pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja", na mwanzo wa utekelezaji wa Mkakati wa uendelezaji wa mambo ya vijijini", China imekuwa ikihitaji kukuza ushirikiano na nje katika mambo ya kilimo. Naibu katibu mkuu wa serikali ya mkoa wa Shandong Bw. Zhang Jijun anasema:

    "Mkoa huo utaimarisha soko la jadi huku ukipanua soko jipya. Vilevile utahimiza kampuni za China kuwekeza na kujenga viwanda katika nchi za nje, kwa kutumia maliasili ya kilimo ya nchi zinazojiunga na pendekezo la 'Ukanda Mmoja, Njia Moja'. Wakati huohuo utainua kiwango cha vifaa na teknolojia za kilimo kwa njia ya kuvutia uwekezaji, wataalamu na teknolojia kutoka nje."

    Bw. Sui Pengfei ameeleza kuwa, kwa kupitia ujenzi wa eneo shirikishi la majaribio la kitaifa la Weifang, China si kama tu itazidi kupanua ufunguaji mlango kwa nje katika mambo ya kilimo na vijiji, bali pia italeta uzoefu mwingi zaidi mzuri kote nchini, akisema:

    "Hayo ni maendeleo yaliyopatikana katika ufunguaji mlango kwenye mambo ya kilimo. Weifang ni mwakilishi mmoja tu, China itahimiza uvumbuzi wa mfumo na hatua ya mageuzi kwa kupitia jukwaa kama hilo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako