• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Li Keqiang kufanya mzungumzo na wakurugenzi wa mashirika makuu ya uchumi ya kimataifa

    (GMT+08:00) 2018-10-30 19:16:21

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang leo hapa Beijing amesema, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang wiki ijayo atafanya mkutano wa tatu wa mazungumzo na wakuu wa taasisi za kimataifa za kiuchumi.

    Lu Kang amesema, Bw. Li atakutana na mkurugenzi wa Benki ya Dunia Jim-Yong Kim, mkurugenzi wa Shirika la Fedha la Kimataifa IMF Bibi Christine Lagarde, katibu mkuu wa Shirika la Biashara Duniani WTO Roberto Azevedo, katibu mkuu wa shirika la ushirikiano na maendeleo ya uchumi Bibi Angel Gurria, mwenyekiti wa baraza la utulivu wa uchumi Mark Carney na naibu katibu mkuu wa Shirika la Kazi la Kimataifa Deborah Greenfield.

    Pamoja na masuala mengine, viongozi hao watajadili mwelekeo wa uchumi duniani, kulinda mfumo wa biashara yenye pande nyingi, uchumi na mageuzi na kufungua mlango ya China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako