• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiwanda cha Midlands chazua siasa

    (GMT+08:00) 2018-10-30 19:38:10

    Siasa zinazozingira umiliki wa kiwanda cha Midlands ambacho ni cha uongezaji ubora mavuno ya viazi katika Kaunti ya Nyandarua zimeibuka. Kiwanda hicho kinamilikiwa na wawekezaji binafsi huku viongozi wa Kaunti hiyo wakishikilia kuwa ni cha umma na ambapo mvutano huo umeishia kupendekezwa kinunuliwe.

    Wachambuzi wa mambo ya uchumi wanasema jambo ambalo halieleweki ni itakuwaje kiwanda hicho kisemwe kwa uhakika kuwa ni cha umma na viongozi walio mamlakani wa Nyandarua wawe ndio wa kusema hivyo, lakini wapendekeze kuwa kinunuliwe kutoka kwa wanaokidai kama wawekezaji wa kibinafsi.

    Kiwanda hicho kinaorodheshwa kama cha pili kwa ukubwa barani Afrika, lakini hakijawahi kuwahudumia wenyeji wa Nyandarua kwa njia ya kuwazidishia mapato ya kilimo chao cha viazi.

    Kiwanda hicho kinadaiwa kujengwa mwaka wa 1987 lakini leseni ya kuhudumu ikatolewa mwaka wea 2004 lakini kikawa na ubadilisho wa umiliki ambapo kiliibuka kuwa cha kibinafsi.

    Hatya hivyo baadhi ya viongozi wamese kiwanda hicho kinafaa kurejeshewa wakulima wa eneo hilo kwa gharama ya ulipaji fidia kwa kima cha Sh500 milioni.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako