• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bei ya mahindi kupanda

    (GMT+08:00) 2018-10-30 19:38:39

    Muungano wa wasagaji nafaka nchini Kenya (UTMA) imetangaza uwezekano wa bei ya unga wa mahindi huenda ikapanda hivi karibuni. UTMA ilisema Jumatatu kwamba wakulima wa mahindi wamekataa kuuza mazao yao wakilalamika kwamba yananunuliwa kwa bei duni. Naibu mwenyekiti wa muungano huu Ken Nyaga alisema hatua hii imesababisha upungufu wa unga, suala ambalo litashinikiza kuongezeka kwa bei yake. Kulingana na muungano huu ni kuwa bei ya pakiti ya kilo mbili itaongezeka kwa Sh25 kutoka bei ya sasa ya Sh75. Serikali kupitia bodi ya kitaifa ya nafaka (NCPB) inanunua gunia la kilo 90 kwa Sh2,300. Bw Nyaga alisema wasagaji wa mahindi wamefikia kiwango cha kushindwa kufadhili taifa kwa unga wa Sh75 pakiti ya kilo mbili kwa sababu ya upungufu wa mahindi. UTMA imeiomba NCPB kuachilia mahindi iliyonayo. Hii ina maana ongezeko hilo litasababisha kilo mbili kuuzwa kwa Sh100.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako