• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ATCL KUREJEA IATA

    (GMT+08:00) 2018-10-30 19:38:57

    Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limeruhusiwa kurejea katika Shirikisho la Mashirika ya Ndege Duniani (IATA), ambapo kuanzia sasa litakuwa na uwezo wa kuuza tiketi zake duniani kote.

    ATCL iliondolewa IATA miaka tisa iliyopita baada ya kulemewa na mzigo wa madeni.

    Tangu kufufuliwa upya kwa shirika hilo 2016, limekuwa likipambana kutaka kurejea upya katika uanachama ili kuepuka kukosa malipo ya tiketi zao hususan katika safari za kimataifa.

    Kurejeshwa kumeanza rasmi mwezi huu. Tayari fomu zote za malipo ambayo hayakufanyiwa kazi au kulipwa wakati ATCL ilipoondolewa katika mfumo, zinapaswa kutumwa upya ACH ili ziweze kushughulikiwa.

    Hatua hiyo ni muhimu kibiashara hususan wakati huu ambao wamelenga kupanua safari zao nje ya mipaka ya Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako