• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Telkom kuwaachisha kazi wafanyakazi 500

    (GMT+08:00) 2018-10-30 19:39:16

    Kampuni ya Telkom nchini Kenya imetangaza kuwa itawapiga kalamu wafanyakazi wake 500, katika mpango wake wa kupunguza gharama ya matumizi.

    Kupitia ujumbe iliotuma kwa vyombo vya habari, kampuni hiyo ilitoa ilani ya siku 30 kwa Wizara ya Leba, kumaanisha kuwa wafanyakazi hao wataondolewa kazini Novemba.

    Hii ni baada ya kampuni hiyo kupinga kuwa ilikuwa ikipanga kuwafuta kazi wafanyakazi wake wiki mbili zilizopita, ambapo ilijitetea kuwa ilikuwa ikilenga kuinua utendakazi na kupanua soko.

    Kampuni hiyo inasemekana kuipa kazi kampuni ya Mckinsey kuifanyia ukaguzi, ambayo ilipendekeza idadi hiyo ya wafanyakazi wachujwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako