• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Serengeti Boys kuusaka ubingwa wa kwanza

    (GMT+08:00) 2018-10-31 08:40:56
    Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 ya Tanzania 'Serengeti Boys' ipo katika maandalizi ya kuelekea mashindano ya vijana ya mataifa yaliyo kusini mwa Afrika 'COSAFA' yatakayofanyika mwezi Disemba.

    Mashindano hayo yatafanyika nchini Botswana ambapo Serengeti Boys inatarajia kushiriki kama mwalikwa. Yatakuwa ni mashindano ya kwanza ya nje ya Afrika Mashariki kwa timu hiyo kushiriki baada ya kumalizika kwa michuano ya CECAFA U-17 Challenge ambayo Serengeti Boys iliondolewa katika hatua ya nusu fainali.

    Serengeti Boys ndiyo wenyeji wa michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana chini ya miaka 17 mwaka 2019, michuano itakayofanyika hapa Tanzania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako