• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Kenya kukopa tena mabilioni ili kujaza pengo la mahitaji ya kifedha

    (GMT+08:00) 2018-10-31 19:24:45
    Serikali ya Kenya inapanga kuchukua mkopo mpya wa Sh287 bilioni.

    Uhaba wa fedha kwenye hazina ya taifa katika bajeti ya mwaka huu ya Sh3 trilioni ulifanya serikali kuongeza ushuru wa bidhaa za mafuta,huduma za mawasiliano ya simu na huduma za kifedha,na ukopaji huu mpya utalazimu serikali kuongeza ushuru zaidi ili iweze kulipa madeni yanayoongezeka.

    Wataalamu wanasema huenda wakenya wakaendelea kukabiliwa na hali ngumu za maisha kwa kipindi kirefu zaidi kwani kuna uwezekano mkubwa wa ushuru na gharama ya maisha kuongezeka tena.

    Habari za mkopo huu mpya zimechipuka wiki chacahe tu baada ya serikali kuongeza ushuru kwa bidhaa za kimsingi kama vile petrol,dawa za kilimo,huduma za utumaji pesa kwa simu.

    Aidha wananchi hivi karibuni watatozwa ushuru wa kugharamia nyumba zitakazojengwa na serikali.

    Katibu wa Wizara ya Fedha, Dkt Kamau Thugge, alinukuliwa akisema serikali itakopa Sh250 bilioni za Eurobond na Sh37 bilioni kutoka kwa mashirika ya kifedha ili kujaza pengo la mahitaji ya kifedha kwenye bajeti ya mwaka huu.

    Ukopaji huo wa Eurobond ni wa tatu kwa serikali ya Jubilee baada ya ule wa Sh200 bilioni mnamo Februari mwaka jana na Sh275 bilioni mnamo 2014.

    Ripoti hizo zilichapishwa na mtandao wa habari za uchumi wa Bloomberg mnamo Jumatatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako