• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ripoti ya Benki ya Dunia yaonyesha mazingira ya biashara ya China yaboreshwa

    (GMT+08:00) 2018-11-01 18:06:13

    Benki ya Dunia jana imetoa ripoti ya mazingira ya biashara ya mwaka 2019, ambayo imeonyesha kuwa mazingira ya kufanya biashara nchini China yameinuka kwa nafasi zaidi 30 kuliko mwaka jana, na kuwa nafasi ya 46 kati ya makundi yote 190 ya kiuchumi.

    Ripoti hiyo inasema, katika mwaka mmoja uliopita, hatua za mageuzi za China kwa ajili ya kuboresha mazingira ya kufanya biashara kwa makampuni yenye ukubwa mdogo na wa kati zimevunja rekodi, na kuchukua nafasi ya kumi kwa nchi zinazoboresha kwa kiasi kikubwa mazingira ya kufanya biashara ya mwaka huu.

    Ripoti hiyo inaonyesha kuwa, kati ya vigezo vikuu 10, China imefanya vizuri katika kuboresha uanzishaji wa makampuni na upatikanaji wa umeme.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako