• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Msumbiji: Umoja wa Mataifa watoa mafunzo ya ukulima bora.

  (GMT+08:00) 2018-11-01 19:02:25

  Nchini Msumbiji mradi wa Umoja wa Mataifa umewezesha maafisa wa ugani kufundisha wakulima namna ya kulima mazao na kuandaa lishe bora na hivyo kuepusha utapiamlo ambao ni tatizo kubwa kwa watoto hususan kwenye jimbo la Cabo Delgado. Mafunzo haya ni sehemu ya mradi wa mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo, IFAD wa kuhakikisha wakazi wa eneo hili wanalima mazao yao kwa ubora zaidi na hatimaye waweze kuboresha lishe kwa watoto wao.

  IFAD inasema asilimia 43 ya watoto nchini Msumbiji wana utapiamlo na katika jimbo hili la Cado Delgado hali ni mbaya zaidi kwa kuwa kiwango cha utapiamlo miongoni mwa watoto ni asilimia 53.

  Baada ya mafunzo wanayopatiwa shambani kuhusu ukulima bora, wakulima hao vile vile wakiwa kwenye vikundi wanafundishwa jinsi ya kuandaa chakula bora.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako