• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asisitiza kuunga mkono maendeleo ya uchumi wa sekta binafsi

    (GMT+08:00) 2018-11-01 19:31:22

    Rais Xi Jinping wa China ameendesha na kuhutubia kongamano la viwanda vya sekta binafsi lililofanyika leo mjini Beijing.

    Rais Xi amesisitiza kuwa, mfumo wa kimsingi wa uchumi wa sekta binafsi huku aina nyingine mbalimbali za uchumi zikipata maendeleo kwa pamoja, sio tu ni sehemu muhimu zinaounda mfumo wa kijamaa wenye umaalumu wa kichina, bali pia ni mahitaji ya lazima ya kukamilisha utaratibu wa uchumi wa soko la kijamaa.

    Amesema hadhi na kazi ya uchumi wa sekta binafsi hazibadiliki katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini China, na mwongozo wa China wa kuhamasisha, kuunga mkono, na kuelekeza maendeleo ya uchumi wa sekta hiyo haubadiliki, pia sera ya China ya kuweka mazingira mazuri na kutoa fursa nyingi zaidi nzuri kwa maendeleo ya uchumi wa sekta binafsi vilevile hayabadiliki. Ameeleza kuwa, katika mchakato mpya wa China wa kujenga kwa pande zote nchi ya kisasa ya kijamaa, sekta hiyo ni lazima ikuzwe na kuelekea katika jukwaa kubwa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako