• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mambo mawili muhimu yanayoandaliwa na China kwa dunia

  (GMT+08:00) 2018-11-01 20:52:47

  Hatua mpya za kufungua mlango za China zimeanza kutekelezwa tokea mwezi Novemba. Kuanzia leo, China itaanza kupunguza kiwango cha ushuru wa forodha kwa bidhaa za aina 1,585 zinazoagizwa kutoka nje. Hii ni hatua mpya ya China ya kupunguza ushuru wa forodha baada ya kuanza kupunguza ushuru wa forodha kwa bidhaa za aina 1,449 zinazoagizwa kutoka nje tangu Julai Mosi. Hadi sasa kiwango cha jumla cha ushuru wa forodha kimepungua kutoka asilimia 9.8 hadi 7.5, na kodi zinazotozwa na kampuni na wateja zinakadiriwa kupungua kwa dola bilioni 8.6 za kimarekani.

  Jumatatu ijayo, Maonesho ya kwanza ya kimataifa ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya China yataanza mjini Shanghai, na yatashirikisha kampuni zaidi ya 3,000 kutoka nchi na sehemu zaidi ya 130 duniani ambazo zitaonesha sura za nchi zao na kupanua soko la kimataifa la biashara, ili kukidhi mahitaji mbalimbali ya wateja wa China na dunia.

  Mbali hayo, ofisi ya siasa ya Kamati kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China imekutana na kutoa uamuzi wa kuongeza nguvu katika kufanya mageuzi na kufunga mlango, kuhimiza kwa hatua madhubuti maendeleo yenye kiwango cha juu,kuendelea kutumia mitaji ya kigeni kwa ufanisi, na kulinda maslahi halali ya kampuni za nchi za nje zilizowekeza nchini China.

  Hizi ni hatua zinazotekelezwa na serikali ya China kwa kufuata hali ya uchumi nchini China. Watu wanatakiwa kuona kuwa China inazidi kufungua mlango kwa dunia, wakati huo huo dunia itaweza kutafuta fursa nyingi zaidi katika mchakato wa China wa kufanya mageuzi na kufungua mlango kwa nje.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako