• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asisitiza uchumi wa sekta binafsi unatakiwa kupata maendeleo makubwa zaidi

    (GMT+08:00) 2018-11-01 21:04:03

    Rais Xi Jinping wa China ameendesha na kuhutubia kongamano la viwanda vya watu binafsi lililofanyika leo mjini Beijing.

    Rais Xi amesisitiza kuwa, mfumo wa kimsingi wa uchumi unaoongozwa na serikali huku aina nyingine mbalimbali za uchumi zikipata maendeleo kwa pamoja, sio tu ni sehemu muhimu zinaounda mfumo wa kijamaa wenye umaalumu wa kichina, bali pia ni mahitaji ya lazima ya kukamilisha utaratibu wa uchumi wa soko la kisoshalisti.

    Rais Xi amesema, katika miaka 40 iliyopita, uchumi wa sekta binafsi umekuwa nguvu isiyokosekana katika kuhimiza maendeleo ya China, na pia umekuwa chanzo muhimu katika kutoa nafasi za ajira, kufanya uvumbuzi wa kisayansi, na kutoa kodi wa taifa, ambao umeonesha umuhimu mkubwa katika maendeleo ya uchumi wa soko la kijamaa, mabadiliko ya madaraka ya serikali, uhamaji wa nguvukazi inayobaki vijijini, na kupanua soko la kimataifa. Sekta hiyo imechangia sana mafanikio yaliyopatikana katika maendeleo ya uchumi nchini China.

    Amesema hadhi na kazi ya uchumi wa sekta binafsi hazibadiliki katika maendeleo ya kiuchumi na kijamii nchini China, na mwongozo wa China wa kuhamasisha, kuunga mkono, na kuelekeza maendeleo ya uchumi wa sekta hiyo haubadiliki, pia sera ya China ya kuweka mazingira mazuri na kutoa fursa nyingi zaidi nzuri kwa maendeleo ya uchumi wa sekta binafsi vilevile hayabadiliki. Ameeleza kuwa, katika mchakato mpya wa China wa kujenga kwa pande zote nchi ya kisasa ya kijamaa, sekta hiyo ni lazima ikuzwe na kuelekea katika jukwaa kubwa zaidi.

    Rais Xi anasema, uchumi wa sekta binafsi ni muundo muhimu katika mfumo wa uchumi wa China. Katiba, na kanuni za chama cha kikomunisti cha China zimehusisha utaratibu huo wa kimsingi na hazitabadilika. Kauli yoyote na kitendo chochote za kukanusha, kushitaki au kuyumbisha utaratibu huo haziendani na mwongozo au sera za chama na nchi. Viwanda vya watu binafsi vitaweza kupata maendeleo bila ya wasiwasi yoyote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako