• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Benki za Kenya kushiriki kwenye Maonesho ya uagizaji bidhaa ya kimataifa ya China

    (GMT+08:00) 2018-11-02 17:04:23

    Maonesho ya kwanza ya uagizaji bidhaa ya kimataifa ya China CIIE yatafanyika hivi karibuni mjini Shanghai, hali ambayo itazinufaisha benki za biashara ya kuvuka mipaka ya nchi. Mkurugenzi wa Benki ya biashara ya Kenya KCB ambayo ni benki kubwa zaidi ya Afrika Mashariki, atakayeshiriki kwenye maonesho hayo Bw. Reginald Kikwai, ameeleza kuwa serikali ya China inafanya juhudi kuongeza uagizaji wa bidhaa kutoka Afrika.

    Kadiri mawasiliano ya biashara kati ya China na Afrika yanavyopata maendeleo kwa kasi, ndivyo maeneo ya ushirikiano wa fedha kati ya pande hizo mbili yanavyozidi kupanuka, hali ambayo imetoa msukumo mkubwa kwa ushirikiano kati ya pande hizo mbili. Benki nyingi za Afrika ikiwemo Benki ya KCB ya Kenya zimeanzisha ofisi nchini China.

    Mkurugenzi wa mikakati wa Benki ya KCB ya Kenya Bw. Reginald Kikwai ameeleza kuwa, hivi sasa Kenya na China zinafanya mawasiliano mengi ya kibiashara. Kampuni za Kenya au kampuni za China zilizoanzisha biashara nchini Kenya, zina mahitaji mengi katika sekta ya utoaji wa huduma za fedha. Anasema: "Lengo la KCB kushiriki kwenye maonesho hayo ni kuongeza uwezo wake katika kuwekeza na kuchangisha fedha, pamoja na kuhimiza mawasiliano ya kibiashara kati ya Kenya na China. Kwa kawaida kampuni za watu binafsi hufanya biashara kupitia benki za biashara, hali ambayo inatuhitaji kuongeza uwezo wetu."

    Licha ya biashara kati ya China na Kenya inaongezeka kwa kasi, bado kuna hali ya kutokuwepo kwa uwiano wa kibiashara. Bw. Kikwai amesema, mkutano wa kilele wa Beijing wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika uliamua kuongeza uagizaji wa bidhaa kutoka Afrika: "Kutokana na juhudi za serikali ya China, bidhaa zinazouzwa nchini China kutoka Afrika zitaongezeka. Ndiyo maana baadhi ya kampuni za Kenya zitashiriki kwenye maonesho hayo. Na zikitaka kufanya biashara, Benki ya KCB itakuwa mwenzi mzuri wa ushirikiano."

    Bw. Kikwai amesema, uhusiano kati ya Kenya na China utazidi kukua kutokana na utekelezaji wa Pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja". Anasema:"Kwa kweli Kenya ni mlango wa 'Ukanda Mmoja, Njia Moja' barani Afrika, wakati Mombasa itakuwa sehemu muhimu ya kuingizwa uwekezaji mkubwa. Tukitupia macho siku za baadaye, hii itakuwa hatua halisi ya kwanza. Tutaimarisha juhudi tulizofanya, na kuwa benki muhimu ya kuunga mkono mawasiliano ya kibiashara kati ya idara za watu binafsi na za umma, na kati ya nchi mbili."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako