• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asisitiza umuhimu wa kushikilia njia ya ujamaa wenye umaalum wa Kichina kwa maendeleo ya wanawake

    (GMT+08:00) 2018-11-02 19:12:36

    Rais Xi Jinping wa China leo amesisitiza umuhimu wa kushikilia njia ya ujamaa wenye umaalum wa Kichina kwa ajili ya maendeleo ya wanawake na kuwakusanya wanawake ili kutimiza mafanikio.

    Rais Xi amesema hayo alipokutana na uongozi mpya wa Shirikisho la Wanawake la China. Akisisitiza umuhimu wa uongozi wa Chama katika kazi za maendeleo ya wanawake, rais Xi amesema ndoto ya China ya kufufua tena taifa inapaswa kuwa dhamira ya kisasa ya maendeleo ya wanawake.

    Amesema juhudi zinatakiwa kufanywa ili kuboresha usawa wa kijinsia, kuwawezesha wanawake kuchukua nafasi kubwa katika sekta zote, na kuwaweka pamoja ili kuchangia katika mageuzi, maendeleo na utulivu wa taifa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako