• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • TRA yataja watu walionufaika na samani zilizoshindwa kulipiwa kodi

  (GMT+08:00) 2018-11-02 19:28:31

  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imewataja watu walionufaika na samani zilizokuwamo katika makontena 20 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda yaliyokuwa yakinadiwa na mamlaka hiyo baada ya kushindwa kuyalipia kodi.

  Katika mgawo wa samani hizo ambazo awali, Makonda alisema zilikuwa kwa ajili ya shule za mkoa wake, TRA imesema haukuambulia chochote kwa kuwa haukuwasilisha maombi.

  Makontena hayo ambayo yalikosa wanunuzi katika minada mitatu iliyoendeshwa kwa nyakati tofauti na kampuni ya udalali ya Yono, yalikuwa na viti, meza na mbao za kuandikia, samani ambazo kwa pamoja zilikuwa zikidaiwa kodi iliyokadiriwa kuwa Sh1.2 bilioni.

  Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi wa TRA, Richard Kayombo amesema makontena hayo yametolewa kwa ofisi za Serikali ambazo zilionyesha uhitaji katika mikoa mitatu, wilaya nne na idara moja ya Serikali. Mikoa hiyo ni Songwe, Geita na Katavi wakati wilaya zilizopata mgawo huo ni Masasi, Nanyumbu na Tandahimba za Mtwara na Liwale ya mkoani Lindi.

  Kugawiwa kwa makontena hayo ni sehemu ya utekelezaji wa Sheria ya Kodi ya Forodha ya Afrika Mashariki ambayo inaelekeza mali zinazokosa mnunuzi ziwekewe utaratibu ikiwamo ule wa kugawiwa bure.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako