• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakenya kuendelea kukabiliwa na wakati mgumu kimaisha

    (GMT+08:00) 2018-11-02 19:28:46

    Wakenya wataendelea kukabiliwa na ugumu wa kimaisha kwa kipindi kirefu zaidi kutokana na uwezekano wa ushuru na gharama ya maisha kuongezeka tena. Hii ni baada ya kufichuka kwamba Serikali inapanga kuchukua mkopo mpya wa Sh287 bilioni.

    Uhaba wa fedha kwenye hazina ya taifa katika bajeti ya mwaka huu ya Sh3 trilioni ulipelekea serikali kuongeza ushuru wa bidhaa mbalimbali ikiwemo mafuta, huduma za mawasiliano ya simu na huduma za kifedha, na ukopaji huu mpya utalazimu serikali kuongeza ushuru zaidi kulipa madeni yanayoongezeka.

    Habari hizi zimechipuka wiki chache tu baada ya Serikali kurundikia mwananchi ushuru kwa bidhaa za kimsingi kama vile petroli, dawa za kilimo, Mpesa na kupiga simu. Pia ushuru wa kugharamia nyumba zitakazojengwa na serikali unatarajiwa kuanza karibuni.

    Katibu wa Wizara ya Fedha, Dkt Kamau Thugge, alinukuliwa akisema serikali itakopa Sh250 bilioni za Eurobond na Sh37 bilioni kutoka kwa mashirika ya kifedha ili kujaza pengo la mahitaji ya kifedha kwenye bajeti ya mwaka huu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako