• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • ATCL yashindwa kuweka wazi safari za Muymbai

    (GMT+08:00) 2018-11-02 19:29:11

    Siku chache tu baada ya shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kurejeshwa katika Shirikisho la Mashirika ya Ndege Duniani (IATA) limeshindwa kuweka wazi tarehe ambayo litaanza safari zake za kwenda Mumbai, India.

    ATCL iliondolewa katika shirikisho hilo mwaka 2009 baada ya kulemewa na mzigo wa madeni, lakini tangu lilipofufuliwa upya 2016 limekuwa likipambana kurejea upya katika uanachama na hivi karibuni limefanikiwa, hivyo kupata fursa ya kuuza tiketi zake kimataifa.

    Mkurugenzi mkuu wa ATCL, Ladislaus Matindi amesema kuwa bado kuna mambo wanayashughulikia ili kuanza safari hizo na muda ukifika wataeleza ili abiria waanze kununua tiketi.

    Julai mwaka huu, ilitangaza safari za kwenda Mumbai zingeanza Septemba, lakini haikuwa hivyo badala yake walieleza itakuwa siku yoyote mwezi Novemba.

    Shauku ya kuanza kwa safari hizo ni kutokana na kutokuwepo kwa ndege za moja kwa moja kwenda katika eneo hilo.

    Mara ya mwisho kufanyika kwa safari za Mumbai zilikuwa zikifanywa na Shirika la Ndege la India (Air India) ambalo sasa halifanyi.

    ATCL imetawala soko la ndani kwa zaidi ya asilimia 24 ikisafirisha abiria katika mikoa 12 na katika nchi za Comoro, Burundi na Uganda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako