• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • EU yatoa shilingi bilioni 5 kama msaada kwa Kenya

    (GMT+08:00) 2018-11-02 19:29:27

    Umoja wa Nchi za Ulaya (EU) umeipatia Serikali ya Kenya msaada wa kiasi cha Sh5 bilioni sawa na bilioni 100 za Kitanzania kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mabasi ya mwendokasi.

    Mradi huo utakaogharimu kiasi cha Sh9.6 billion ni kwa ajili ya jiji la Nairobi ambapo ndipo yalipo makao makuu ya nchi hiyo ya Kenya.

    Mradi huo ulizinduliwa mwaka 2015 na Rais Uhuru Kenyatta, ambao umeanza kwa kujengwa barabara za mabasi hayo ikiwa ni pamoja na ununuzi wa mabasi hayo. Balozi wa EU nchini Kenya Stefano Dejak amesema kwamba fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuendeleza mradi huo ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu itakayochukua muda wa miaka mitatu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako